Connect with us

Habari za Kimataifa

ZIDANE ATAJA ATAKAOTUA NAO MAN U AKICHUKUA MIKOBA YA MOURINHO

Kocha wa zamani wa Real Madrid ya Hispania, Zinedine Zidane ambaye kwa kipindi hiki hana timu, ametaja baadhi ya wachezaji ambao anaweza kuwatumia iwapo atafanikiwa kuwa kocha wa Klabu ya Manchester United ya England ikiwa atapata ajira kikosini hapo.
Zidane ambaye ameipa mafanikio makubwa Madrid, inayojulikana kama Los Blancos, amewataja wachezaji Kroos, Thiago Alcantara, James Rodriguez na Edinson Cavani ambao alisema wako tayari kuungana naye katika Klabu ya Manchester iwapo atamrithi kocha wa sasa Jose Mourinho.
“Ni kweli, nitarejea tena kwenye kufundisha, kwani ndiyo kazi ambayo nimeifanya siku zote hadi sasa,” alisema Zidane alipohojiwa na kituo cha televisheni cha TVE.
Mourinho hivi sasa yuko chini ya shinikizo kufuatia klabu hiyo kufanya vibaya msimu uliopita na ambapo hadi sasa imepoteza michezo miwili miongoni mwa minne iliyocheza katika Ligi Kuu ya England.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kimataifa