Connect with us

Habari za Kitaifa

YANGA YAFUNGUKA KUHUSU RATIBA YA LIGI KUU ‘KUWABEBA’ WAO

Kurejea kwa Ligi Kuu Bara wikiendi hii kunaonekana kupokewa vizuri na Yanga kutokana na ratiba kuonekana imekaa vizuri kwao.

Yanga itashuka uwanjani wikiendi hii kucheza dhidi ya Stand United lakini ratiba inaonyesha kuwa timu hiyo itakuwa na michezo mingi nyumbani, yaani jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Usajili wa Yanga, Hussein Nyika, amesema wao uongozi wameipokea vizuri ratiba hiyo.

Ratiba inaonyesha kuwa Yanga watakuwa na michezo saba nyumbani na 4 ugenini katika michezo 11 inayofuata, Nyika amesema wao hilo hawalitilii maanani na badala yake watapambana kuhakikisha wanavuna alama zote.

Nyika anaamini hiyo si fursa bali ni mapambano kama fainali kwa kila mechi maana kuna faida na hasara zake unapopata ratiba ya aina kaa hiyo.

Yanga itacheza dhidi ya Stand United, Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wake wa pili baada ya mechi ya kwanza na Mtibwa Sugar ambao walishinda kwa mabao 2-1.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa