Connect with us

Habari za Kimataifa

WAPINZANI WA SIMBA, ASANTE KOTOKO KUTUA DAR KESHO JUMANNE, WAPO FULL NONDO

Kuelekea Tamasha la Simba Day ambalo linatarajiwa kufanyika keshokutwa Jumatano, wapinzani wa SImba katika tamasha hilo, Asante Kotoko wa Ghana wanatarajiwa kuwasili nchini kesho.

Asante Kotoko itawasili kesho Jumanne kwa ajili ya tamasha hilo ambalo linaadaliwa na Simba na kufanyika kila mwaka kabla ya kuanza kwa msimu.

Safari hii Simba inaingia katika tamasha hilo ikiwa bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kotoko ambao wapo nafasi ya 4 katika msimamo wa Ligi Kuu Ghana wakiwa na tofauti ya alama 3 dhidi ya Ashanti Gold iliyo kwenye nafasi ya kwanza huku kila timu ikicheza mechi 15, wamekubali mwaliko wa kuja nchini.

Haji Manara ambaye ni Ofisa Habari wa Klabu ya Simba amethibitisha juu ya ujio huo kwa kusema kuwa Kotoko watakuja wakiwa na ‘full mkoko’.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kimataifa