Connect with us

Habari za Kitaifa

(VIDEO) EXCLUSIVE: CHAMA MZAMBIA WA SIMBA NITAFANYA MAAJABU MSIMBAZI

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba, jana walifanikiwa kubeba taji la la Ngao ya Hispani baada ya kuifunga Mtibwa Sugar, mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Simba imepata mabao yake kupitia kwa Meddie Kagere aliyefunga dakika ya 29 na Hassan Dilunga 45+3 wakati bao pekee la Mtibwa Sugar likifungwa na Kelvin Kongwe 33.

Kukamilika kwa mchezo huo ni ishara sasa ya kufunguliwa rasmi kwa michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara inayorajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22.

Mara baada ya mchezo huo Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila alikiri kuwa wapinzani wao walikuwa vizuri lakini hata vijana wake wameonyesha uwezo mzuri huku kiun go mpya wa Simba, Mzambia Chama Clatou akisema anaamini anaweza kuwa na msimu mzuri licha ya kuwa amekuwepo Tanzania kwa muda mfupi.

Bonyeza video kutazama alichokisema kiungo huyo ambaye amekuwa ni kipenzi cha mashabiki wa Simba ndani ya muda mfupi aliokuwepo klabuni hapo:

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa