Connect with us

Habari za Kimataifa

TETESI ZA USAJILI WA ULAYA, WAMO 0KUHUSU POGBA, MARTIAL, ZIDANE

Hizi ni tetesi mbalimbali zinazohusua usajili na masuala mengine ya soka katika Bara la Ulaya kutoka vyanzo mbalimbali:
BEKI Jerome Boateng, 30, amemwambia Jose Mourinho kuwa amekataa ofa ya kujiunga na Mashetani Wekundu kwa sababu haoni kuwa kuhamia Manchester United akitokea Bayern Munich kama kupiga hatua ya maendeleo. (Mirror)

MSHAMBULIAJI Marcus Rashford anataka kusalia Manchester United na kupambana kupata nafasi katika kikosi cha kwanza. Hatahivyo kama atashindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza basi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 atalazimika kufanya maamuzi magumu mwishoni mwa msimu.
(Sun)

KOCHA wa Manchester United Mourinho “ameshindwa kumvumilia” winga wa klabu hiyo Anthony Martial mwenye umri wa miaka 22. Martial anatarajiwa kuondoka United na kujiunga na timu nyengine ya ligi kuu ya England. Klabu za Arsenal na Tottenham zimeonesha nia ya kumsajili raia huyo wa Ufaransa. (Express)

PAUL Pogba “aliahidiwa” na wakala wake wakati anarejea Manchester Unite akitoka Juventus kuwa angejiunga na Barcelona au Real Madrid mara baada ya kumalizika kwa msimu.
(Manchester Evening News)

RAIS wa Real , Florentino Perez ameghadhabika baada ya kusikia mipango ya kocha wa zamani wa klabu hiyo Zinedine Zidane kuwa anataka kuinoa Manchester United.
(Express)

CHELSEA wapo katika hatihati ya kumpoteza kiungo wa Uhispania Cesc Fabregas, 31, na kuelekea Inter Milan ama AC Milan kama mchezaji huru mwezi Januari kutokana na mkataba wake kukipiga katika Dimba la Stamford Bridge kufikia kikomo mwisho wa msimu. (Express)

KIUNGO wa Arsenal Aaron Ramsay, 27, amesema yupo katika rada za Klabu ya AC Milan. Mkataba wa kiungo huyo na Arsenal unamalizika mwisho wa msimu.
(Sun)

Kiungo mchezeshaji wa Lyon Nabil Fekir, 25, ameachana na fikra za kukwama kwa uhamisho wake – lakini hilo halijamkatisha tamaa ya kufikiria kuchezea Ligi ya England katika siku za usoni.
(Mirror)

WINGA Willian amesema hakutaka kabisa kuhama Chelsea katika kipindi hiki licha ya kutakiwa na Manchester United na kupokea ofa mara tatu kutoka Barcelona. Raia huyo wa Brazil mwenye miaka 30 anatumai kusalia Chelsea kwa miaka mitano Zaidi. (Sky Sports)

JUVENTUS watajaribu kumnunua tena nyota wa Ufaransa anayeichezea Manchester United Paul Pogba mwenye miaka 25 mwezi Agosti mwaka ujao. Mabingwa hao wa Italia pia wanataka kumnunua beki wa Brazil, Marcelo, mwenye miaka 30 ambaye kwa sasa huwachezea Real Madrid.
(Tuttosport)

BARCELONA wanajiandaa kuwanunua mabeki kamili wa Uhispania Nacho Monreal, 32, na Alberto Moreno, 26, ambao huchezea Arsenal na Liverpool mtawalia.
(Mundo Deportivo)

KIUNGO wa kati wa Ujerumani anayechezea Manchester City Ilkay Gundogan, 27, yuko radhi kuwakataa Barcelona ambao wanataka kumnunua mwezi Januari na badala yake kuanzisha mazungumzo kuhusu mkataba mpya katika klabu hiyo ya Etihad.
(Sun)

WINGA wa Liverpool kutoka Serbia Lazar Markovic, 24, ameshushwa hadhi na kulazimishwa kushiriki mazoezi na timu ya vijana wa chini ya miaka 23 katika klabu hiyo. Markovic amechezea Liverpool mechi 19 Ligi ya Premia tangu ajiunge nao kwa uhamisho wa £20m kutoka Benfica mwaka 2014.
(Liverpool Echo)

MSHAMBULIAJI wa Everton na England Theo Walcott, 29, anatarajiwa kuikosa mechi ya Ligi ya Premia Jumapili dhidi ya West Ham baada ya kuumia ubavuni. Hata hivyo, Wacott anatarajiwa kuwa sawa kucheza dhidi ya klabu yake ya zamani Arsenal mnamo 23 Septemba. (Telegraph

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kimataifa