Connect with us

Habari za Kitaifa

SIMBA WAWAFUATA NDANDA FC KWA PIPA, WAMESHATUA MTWARA

Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kurejea kuanzia kesho Ijumaa na kuendelea wikiendi hii yaani Jumamosi na Jumapili, kuelekea mechi hizo, kikosi cha Simba kimepanda ndege leo Alhamisi kuelekea Mtwara kwa ajili ya mtanange dhidi ya Ndanda FC.
Simba ambao makao makuu yao ni jijini Dar es Salaam wanatarajiwa kushuka uwanjani Jumamosi ya keshokutwa kukipiga na wenyeji wao hao kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kuelekea mechi hiyo, uongozi wa Simba umesema asilimia kubwa ya maandalizi ya mchezo huo yameenda vizuri na kikosi kimewasili salama Mtwara na kimeshaanza maandalizi ya mchezo huo.
Upande wa Kocha Mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems, amesema dhamira yake ni kupata ushindi, hivyo ameahidi kuzipigania vilivyo ili kuiweka Simba kileleni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa