Connect with us

Habari za Kimataifa

SIMBA WANAREJEA KWA KISHINDO BAADA YA KUFANYA KWELI BONGO

Kikosi cha Simba ambacho kilikuwa nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa 2018/19, kimeanza safari ya kurejea nchini Tanzania.

Simba imemaliza kambi yake ya siku kadhaa ambapo wlaipata nafasi ya kucheza pia mechi za kirafiki, hivyo wanarejea nchini kujiandaa kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar baadaye mwezi ujao.

Picha kadhaa zilisambazwa zikiwaonyesha wachezaji wa timu hiyo wakiwa katika purukushani za kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ataturk Istanbul nchini Uturuki tayari kurejea nyumbani.

Kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba watakipiga na Asente Kotoko ya Ghana katika Tamasha la Simba Day.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kimataifa