Connect with us

Habari za Kitaifa

SIMBA KUVUNA Sh 20.8M KILA MWEZI ZA UWANJA WA BUNJU

Kuelekea Tamasha la Simba Day ambalo litafanyika kesho Jumatano, rasmi sasa Klabu ya Simba imeamua kuweka wazi juu ya mkataba mpya wa udhamini wao.

Simba imeeleza kuwa mkataba wao huo ni wa Kampuni ya Utengenezaji vinywaji ya A One Products kupitia kinywaji cha Mo Energy Drink.

Mkataba huo una thamani ya shilingi milioni 250. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Mwasala Masoud amesema fedha hizo zitahusika na Simba kwa ajili ya shughuli mbalimbali ndani ya klabu.

Kwa kiwango hicho inamaanisha kwa kuwa ni mkataba wa mwaka mmoja, inaonyesha ni kama kila mwezi watakuwa wanaingiza Sh milioni 20.8 kwa muda wa miezi 12 wa mkataba huo.

Mwasala ameeleza kuwa kinywaji cha Mo Energy kitakuwa kinaiwakilisha Kampuni ya A One kutokana na utengenezaji wa bidhaa zake ambazo inazalisha.

Ameeleza kuwa mkataba huo unaweza ukaongezwa tena baada ya kufikia ukingoni baada ya miezi 12 ijayo kumalizika.

Baada ya A One na Simba kusaini mkataba huo, Kaimu wa Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again, amesema fedha hizo ambazo ni milioni 250 zitaenda katika mradi wa ujenzi wa Uwanja Bunju.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa