Connect with us

Habari za Kimataifa

SAMATTA AFUNGUKA KUHUSU MIPANGO YA KUMILIKI NDEGE YAKE BINAFSI

Staa wa timu ya soka ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta amefunguka kuhusu ndoto yake ya kumiliki ndege binafsi.

Akitumia ukurasa wake binafsi wa Instagram, Samatta ameonyesha nia hiyo alipokuwa akipiga picha karibu ndege iliyokuwa na nembo ya klabu yake ya Genk kisha ndipo akaelezea ndoto yake hiyo.

Akifafanua zaidi straika huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameandika hivi:

“Ndoto za kumiliki private jet zimeanza baada ya kupiga picha hii 🤨 siyo kila ndoto inaweza kutimia ila, acha vita ianze”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kimataifa