Connect with us

Habari za Kitaifa

KOCHA YANGA ATABIRI TIMU YAKE KUPATA KIPIGO KINGINE KUTOKA KWA GOR MAHIA

Yanga ilipata kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika, Jumanne ya wiki hii, bado gumzo ni juu ya kiwango kilichoonyeshwa na Yanga.

Akizungumzia mchezo huo Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kilichotokea katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Moi Kasarani mjini Nairobi kimetokana na wachezaji kutokuwa fiti na anaona kwamba wana nafasi ndogo ya kufanya vizuri katika mchezo wa marudio dhidi ya timu hiyo.

Kocha huyo amefunguka akisema: “Tulisafiri na wachezaji wengine kwa sababu kukwepa adhabu ambayo tungepewa na Caf

(Shirikisho la Soka Afrika) kama tungeenda na wachezaji wachache. Na kuhusu mechi ijayo pia sidhani kama tutaweza kushinda kwa sababu siku ni chache na wachezaji wale wazoefu hawapo kwenye timu.

“Kuhusiana na wachezaji Ngassa (Mrisho) na Feisal ‘Fei Toto’ wao tutashindwa kuwatumia kwa sababu kanuni za Caf zinataka majina ya wachezaji wapya yawasilishwe siku 14 kabla ya mechi, lakini ukiangalia mechi yetu ijayo (itachezwa Julai 29) itakuwa muda wa siku hizo haujafika, hivyo wachezaji hao sitaweza kuwatumia kabisa.”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa