Connect with us

Habari za Kitaifa

KAULI YA SINGIDA UNITED KUHUSU KOCHA MOROCCO KUONDOKA KAZINI

Wiki mbili zilizopita kuliibuka taarifa kuwa Kocha Mkuu wa Singida United, Hemed Morocco amepata dili nje ya nchi na anatarajiwa kwenda kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ana madai yake klabuni kwake.

Hilo halikujibiwa vizuri, ukimya ukatawala, lakini juzi lilibuka na ikaelezwa kuwa kocha huyo mwenyeji wa Zanzibar, yupo njje ya klabu hiyo kwa sababu zile zile za maslahi.

Mtu wa karibu wa kocha huyo alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akidai kuwa Morocco ana madai yake na hajalipwa ndiyo maana

Alipoulizwa juu ya taarifa hizo, Mkurugenzi wa Singida, Festo Sanga amedai kuwa taarifa hizo siyo za kweli.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya taarifa kusambaa mitandaoni zikieleza Morocco ameamua kuikacha Singida kutokana na kutotimiziwa stahiki zake muhimu ambazo awali walikubaliana.

Sanga amekanusha huku akisema Morocco bado ni Kocha wa Singida na sasa yupo Zanzibar huku akieleza baadaye atarejea kuendelea na majukumu yake ya kuinoa timu kama kawaida.

Kocha huyo alichukua nafasi hiyo baada ya Hans van der Plujim kupata dli la kuifundisha Azam FC.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa