Connect with us

Habari za Kitaifa

HUU HAPA UZI MPYA WA SIMBA ,BOCCO, OKWI ,GYANI NA KOTEI WALIVYOUTAMBULISHA

Klabu ya Simba imetambulisha jezi zake mpya zitakazotumia kwa msimu wa 2018/19.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema jezi hizo zitaanza kuuzwa kuanzia kesho majira ya saa 10 kamili jioni.
Jezi nyeupe zitakuwa zinatumika kwa mechi za ugenini na nyekundu zitatumika kwa mechi za ugenini.

Simba imetambulisha jezi hizo zenye nembo ya mdhamini mkuu SportPesa na Mo Energy Drink ambao ni wadhamini wapya waliotangazwa leo kwa kuingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi milioni 250.
Aidha, kwa upande mwingine kuelekea tamasha la Simba Day Jumatani hii ambapo Simba itacheza dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, Manara amewaomba mashabiki na wanachama wa Simba wajitokeze kwa wingi Uwanjani wakiwa wamevalia jezi mpya ili kuipa hamasa timu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa