Connect with us

Habari za Kitaifa

HIZI NDIYO SABABU KWA NINI TRY AGAIN AMEKATAA KUGOMBEA URAIS WA SIMBA

Kaimu Rais wa Klabu ya Simba Salim Abdallah ‘Try Again’ amenithibitishia kwamba hana mpango wa kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya klabu hiyo ikiwa ni pamoja na urais/uenyekiti.

Salim ametaja sababu ambazo zimefanya asigombee na kuamua kujiweka pembeni ya mchakato huo.

“Chini ya uongozi wangu nikiwa nakaimu nafasi ya urais nimesimamia mabadiliko ya uendeshaji wa klabu kutoka mfumo wa wanachama kwenda mfumo wa hisa. Endapo nitagombea inaweza kutafsiriwa kuwa nilifanya hivyo nikiwa najitengenezea mazingira ya kuja kuongoza baadaye.

“Nimefanikisha mchakato huo na sasa Simba ipo kwenye mfumo mpya inatosha, nikigombea ungozi ndani ya Simba kutakuwa na mgongano wa kimasahi.”

“Wakati naingia kwenye uongozi, kwa muda mrefu Simba ilikuwa haijashinda ubingwa wa ligi ya Tanzania. Nashukuru msimu uliopita nimeweza kuiongoza kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.”

“Nadhani kwa hayo niliyofanya nikiwa kiongozi ndani ya Simba inatosha, ni wakati wa kuwapisha watu wengine waje kuendelea nilipoishia mimi.”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa