Connect with us

Habari za Kitaifa

HII NDIYO SABABU YA JOHN BOCCO KUIKOSA ASANTE KOTOKO LEO…

Simba itashuka uwanjani leo Jumatano katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana lakini itamkosa nahodha wake, John Bocco.

Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa 2018/19 ambapo Simba iliyokuwa nchini Uturuki kwa siku kadhaa ikiwa kambi, itamkosa Bocco ambaye inaelezwa kuwa afya yake siyo nzuri.

Taarifa kutoka ndani ya Simba ambayo inanolewa na Kocha Patrick Aussems imeeleza kuwa Bocco bado ni majeruhi, hivyo katika mechi dhidi ya Asante Kotoko hataweza kuwa sehemu ya kikosi.

Ikumbukwe Bocco hakuweza kucheza mchezo hata mmoja wa kirafiki kati ya mbili walizocheza wakati Simba ikiwa nchini Uturuki kwa kambi ya wiki mbili.

Mtanange huo wa leo unatarajiwa kuanza saa kumi jioni lakini kuanzia saa sita mchana kutakuwa na purukushani na harakati mbalimbali kwa ajili ya tamasha hilo linalofanyika kila mwaka mara moja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa