Connect with us

Habari za Kitaifa

HII NDIYO KAULI YA CHUJI KUHUSU COASTAL UNION NA LIGI KUU

Kiungo Athuman Idd ‘Chuji’ ambaye amesajiliwa Coastal Union ameeleza kuwa anaamini watakuwa na msimu mzuri, hivyo amewataka mashabiki wao kuw ana subira na kusubiri mambo mazuri.
Kiungo huyo wa zamani wa Yanga na Simba amesema anakiamini kikosi chao na kudai kuwa kuongezeka kwa timu katika Ligi Kuu Tanzania Bara kutaongeza ugumu na ushindani wa ligi hiyo.
Chuji alipambana kwa nguvu kubwa kuisaidia timu ya Coastal Union kurejea Ligi Kuu Bara kwa mara nyingine.
Kiungo huyo amesema kujipanga vyema kwa sasa ni muhimu sababu msimu mpya utakuwa ni mgumu na wenye ushindani kwa kiasi kikubwa tofauti na nyuma.
“Unajua kuelekea msimu mpya tunatakiwa kujipanga kweli ushindani utakuwa mkubwa sababu kwanza timu zimeongezeka na ina maana tutacheza mechi nyingi zaidi sio kwenye ligi tu kuna FA hivyo maandalizi mazuri ni muhimu,” calisema Chuji.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa