Connect with us

Habari za Kitaifa

FEDHA ZA UBINGWA WA FA ZA MTIBWA SUGAR, KIZUNGUMKUTI, TFF YAFUNGUKA

Baada ya madai kuwa Mtibwa Sugar wamelalamikia kutopewa fedha zake za mshindi wa Kombe la FA za msimu uliopita, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeulizwa juu ya suala hilo.

Mkurugenzi wa Mashindano, Salum Madadi amesema kwa namna anavyowafahamu Mtibwa Sugar hawawezi wakatoa kauli kama hiyo.
Madadi ameeleza kuwa Mtibwa wamekuwa ni watu wastaarabu hivyo haamini kama wanaweza kuzungumza kwenye vyombo vya habari wakilalamikia kuwa hawajapewa fedha zao.

Madadi ameeleza kuwa kwa sasa hatakuwa na kuzungumza zaidi na badala yake watakuja na tamko lao kuhusiana na fedha hizo siku za usoni.

Mtibwa inadai kitita cha fedha ambazo ni shilingi za kitanzania, milioni 50 baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United Juni 2 2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa