Connect with us

Habari za Kitaifa

COASTAL UNION YA ALIKIBA YAZUIWA KUFANYA MAZOEZI UWANJA WA KARUME

Kikosi cha Coastal union ambacho kinashiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara kimeshindwa kufanya mazoezi asubuhi ya leo kwenye Uwanja wa Karume uliopo Ilala jijini Dar es Salaam.

Coastal ambayo makao makuu yake ni Tanga, ipo jijini Dar kwa ajili ya mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Afeican Lyon, kesho Ijumaa, waliomb a kuutumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi ya leo Alhamisi asubuhi lakini ikashindikana kutokana na kuwa na matumizi mengine.

Mashabiki wengi walifika uwanjani hapo ili kumuona mchezaji mpya wa Coastal, Alikiba ambaye pia ni mwanamuziki akishiriki katika mazoezi hayo.

Alikiba alisajiliwa hivi karibuni na timu hiyo akiwa mchezaji huru lakini bado hajacheza mechi hata moja kutokana na kubanwa na kazi zake za kisanii.

Ilidaiwa kuwa timu hiyo imepangiwa kufanya mazoezi hapo tena, leo jioni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa