Connect with us

Habari za Kimataifa

CHELSEA KUWEKA REKODI YA USAJILI KWA MSAIDIZI WA DE GEA

Chelsea wamepiga hatua nzuri katika mazungumzo yao ya kutaka kumnunua kipa Kepa Arrizabalaga kutoka Athletic Bilbao ya Uhispania katika uhamisho ambao utavunja rekodi ya nunua ya ununuzi wa golikipa.

Kipa huyo mwenye miaka 23 ambaye anaweza kusajiliwa kwa pauni milioni 71, anatarajiwa kununuliwa kujaza nafasi ya Thibaut Courtois ambaye anaonekana kutokuwa tayari kusalia katika klabu hiyo ya Stamford Bridge.

Ikiwa dili hilo litakamilika, inamaanisha kuwa litakuwa kubwa zaidi ya lile la pauni 66.8m ambazo Liverpool walilipa mwezi Julai kumchukua kipa wa Brazil, Alisson.

Courtois, ambaye huchezea timu ya taifa ya Ubelgiji, bado hajarejea mazoezini huku tetesi zikimhusisha na kuhamia Real Madrid.

Mchezaji huyo mwenye miaka 26 alikuwa ametarajiwa kujiunga na wenzake kwa mazoezi ya kuanza msimu Jumatatu lakini hakufika.
KEPA KIPA MSAIDIZI WA DE GEA
Kepa ni kipa nambari mbili katika timu ya taifa ya Uhispania, akiwa nyuma ya kipa wa Manchester United David de Gea, na amechezea timu ya taifa mechi moja pekee.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kimataifa