Connect with us

Habari za Kitaifa

AZAM FC IMESHATUA SHINYANGA, INAISUBIRI KWA HAMU MWADUI FC

Kikosi cha Azam FC kimeshawasili salama mkoani Shinyanga tayari kabisa kwa mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Mwadui utakaofanyika Uwanja wa Mwadui Complex kesho Ijumaa kuanzia saa 8.00 mchana.

Azam FC iliwasili jana ikiwa na kikosi chake kamili isipokuwa kiungo mshambuliaji, Tafadzwa Kutinyu, atayeungana na timu muda wowote kaunzia sasa akitokea kwenye majukumu ya timu ya timu yake ya taifa ya Zimbabwe.

Wachezaji wengine wa Azam FC ambao hawajaungana na timu ni mshambuliaji Wazir Junior pamoja na beki Yakubu Mohammed na Donald Ngoma, ambao wanaendelea na programu ya kujiweka fiti kabla ya kuanza kucheza mechi za ushindani wakitoka kwenye majeraha huku Joseph Kimwaga, akiwa majeruhi.

Mara baada ya kuwasili, kikosi hicho kinatarajia kufanya mazoezi leo Jumatano jioni kwenye Uwanja wa Kambarage mjini hapa kabla ya kesho Alhamisi kujifua tena katika Uwanja wa Mwadui itakaochezea mchezo huo, unaotarajia kuwa mkali na wa aina yake.

Azam FC inayodhaminiwa na kinywaji safi cha juisi cha African Fruti, maji safi ya Uhai Drinking Water na Tradegents Tanzania Limited, hadi sasa inashika nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa na pointi sita ikishinda mechi mbili za awali ilizocheza, ikizidiwa pointi moja na Mbao inayoongoza kileleni ikiwa na pointi saba lakini ikicheza mechi moja zaidi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa