Connect with us

Habari za Kimataifa

ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN NI MAJANGA, ATAKUWA NJE YA UWANJA MSIMU MZIMA

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Alex Oxlade-Chamberlain anatarajiwa kukosa michezo yote ya msimu ujao wa 2018/19 kutokana na tatizo la goti.

Ripoti kutoka Liverpool imeeleza kuwa staa huyo mwenye umri wa miaka 24, alipata majeraha makubwa wakati wa mchezo dhidi ya Roma, Aprili, mwaka huu na hivyo kulazimika kufanyiwa uchunguzi mkubwa.

Ameumia katika mguu wa kulia na vipimo vinaonyesha amevunjika sehemu kadhaa katika maungio ya goti lake.

Madaktari walimfanyia upasuaji na kumwambia kuwa anatakiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi 12 kutokana na huduma aliyopatiwa.

Awali baada ya kuumia klabu haikutaka kutoa taarifa sahihi kwa wachezaji wenzake kwa kuhofia kuwavuruga kisaikolojia na kuvuruga msimu wao uliopita, lakini baada ya miezi kadhaa sasa wameamua kuweka wazi kuhusu ukubwa wa jeraha hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kimataifa