Connect with us

Habari za Kitaifa

RATIBA YA TAMASHA LA SIMBA DAY HII HAPA

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema shughuli nzima za tamasha kubwa la Simba Day leo zitaanza saa 6 kamili mchana.

Manara ameeleza tiketi ambazo zinauzwa kwa njia ya elektroniki kupitia selcom kadi zitakuwa zinapatika kuanzia asubuhi mapema kabisa huku mageti ya kuingialia yakifunguliwa majira ya saa 3.
Akiongezea, Ofisa huyo amesema kikosi B cha Simba kitacheza na Dodoma FC ya Dodoma inayonolewa na Mwanachama wa Simba, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ kabla ya mechi ya wakubwa kupigwa ambayo itaanza majira ya saa 10 jioni.

Kuelekea mechi hiyo itakayowatambulisha wachezaji wa Simba watakaotumika kwa msimu ujao, mgeni rasmi ndani ya tamasha hilo atakuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaaliwa.

Simba inaingia katika tamasha hilo kubwa kukipiga na Asante Kotoko kutoka Ghana ambayo imewasili jana majira ya saa 2 asubuhi nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Habari za Kitaifa