Usajili

WEST HAM WANAMTAKA BENITEZ KUBEBA MIKOBA YA MOYES

Klabu ya West Ham imeanza mikakati ya kumpata Rafa Benitez ili awe kocha wao akitokea Newcastle United, hatua ambayo imekuja baada ya David Moyes kuondoka klabuni hapo.

Moyes ameondoka West Ham, juzi Jumatano lakini hakuwa na furaha kwa jinsi alivyoondoka kwa kuwa kuna baadhi ya mambo hakufanyiwa na uongozi. 

Benitez amekuwa na maisha magumu Newcastle kutokana na uongozi kutomtimizia mahitaji yake hasa katika usajili lakini West Ham wanaonekana kuwa tayari kuwekeza.