Usajili

ATLETICO MADRID YAMUAGA VIZURI TORRES, YAMPA KOMBE LA EUROPA LEAGUE

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya mshambuliaji mkongwe Fernando Torres kuondoka ndani ya Atletico Madrid, timu hiyo imefanikiwa kubeba ubingwa wwa Europa League usiku wa kuamkia leo.

Mabao mawili ya Antoine Griezman dakika ya 21 na 49 Griezman pamoja na lile la Gabi dakika ya 89 yaliiwezesha timu hiyo kubwa bingwa baada ya kuifunga Marseille katika mchezo wa fainali.

Matokeo hayo yamekuwa clean sheet ya 200 kwa Kocha Diego Simeone ndani ya Atletico Madrid. 

Torres ambaye ameichezea timu hiyo katika vipindi viwili, ametwaa taji lake la kwanza kubwa akiwa kikosini hapo baad aya kucheza mechi 403 huku akiwa njiani kuondoka baada ya mkataba wake kuelekea kumalizika mwishoni mwa msimu huu.