Usajili

YANGA WAFUNGUKA BAADA YA KUSIKIA TAARIFA ZA RAIS MAGUFULI KUWAKABIDHI SIMBA KOMBE

 Siku Moja baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kutuma maombi ya kumuomba Rais wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuwa mgeni rasmi katika mechi ya Simba dhidi ya Kagera Sugar, Wanayanga wamezungumza juu ya maamuzi hayo.

TFF ilichukua maamuzi hayo kupitia kwa rais wake, Wallace Karia, ambapo maombi yao yalikubaliwa na sasa Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika mchezo huo wa Jumamosi ya wiki hii ambapo unatarajiwa kuanza saa nane mchana.

Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga nchini, Bakili Makele ndiye ambaye amezungumza juu ya maamuzi hayo. 

Amesema yeye pamoja na Wanayanga hawana kinyongo na suala hilo kutokana na ombi hilo la TFF kumuhitaji Rais Magufuli awe mgeni rasmi.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya maneno ambayo yamekuwa yakielezwa kuwa Yanga imepatwa na kinyongo sababu bingwa wa nchi amekuwa Simba, jambo ambalo amesema si sahihi.

Makele amefunguka kwa kueleza Simba ndiye bingwa wa nchi kwa sasa na wanastahili pongezi kutokana na kazi kubwa waliyoifanya msimu huu.