Usajili

BAADA YA UBINGWA, PEP GUARDIOLA AWA KOCHA BORA WA PREMIER LEAGUE

Pep Guardiola ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu England kufuatia kuiwezesha Manchester City kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo.

Kocha huyo raia wa Hispania ameiwezesha Man City kufikisha pointi 100 katika ligi hiyo na kushinda jumla ya mechi 32 huku akipoteza michezo miwili.

Mbali na ushindi huo, kikosi chake kimeweza kufunga jumla ya mabao 106 na kikiweza kwenda sare katika michezo minne.

Guardiola alijiunga na Manchester City msimu wa 2016/17 akitokea Bayern Munich inayoshiriki ligi ya Bundesliga.