Usajili

KAPOMBE: BAO NILILOFUNGA NI MAALUM KWA MWANANGU ALIYEZALIWA HIVI KARIBUNI

Beki na kiungo Simba, Shomari Kapombe ambaye aliifungia timu yake bao pekee la ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom, jana dhidi ya Singida United ameeleza kuwa bao hilo ni zawadi kwa mtoto wake.

Kapombe alishangilia kwa aina ya kubembeleza huku akipewa sapoti na wenzake kadhaa ambapo alipomaliza mchezo huo kwenye Uwanja wa Namfua alisema ni maalum kwa mtoto wake mchanga ambaye amempata hivi karibuni.

“Zawadi ya goli hili kama mlivyoona nilipofunga nilishangilia kwa sababu nimepata mtoto wa kike, nashukuru Mungu kwa kunipa zawadi hii” alisema Shomari Kapombe.