Usajili

ATLETICO MADRID YAITOLEA POVU BARCELONA KISA NI GRIEZMANN

 Atletico Madrid inasema kuwa imechoshwa na kero la Barcelona la kumuwania mshambuliaji wao, Antoine Griezmann, na imetaka mabingwa hao wa La Liga kuwa na heshima.

Akizungumza siku ya Jumatatu, rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu alisema kuwa alikutana na ajenti wa Griezmann mapema msimu huu

Atletico iliiripoti Barcelona kwa Fifa kuhusu madai ya kumnyatia mchezaji huyo wa Ufaransa mnamo Disemba 27.

"Tumechoshwa na tabia mbaya ya Barcelona," alisema afisa mkuu mtendaji wa Atletico Miguel Angel Gil Marin.

Marin aliongezea kuwa matamshi ya Bartomeu kuhusu Griezmann kabla ya mechi ya fainali ya ligi ya Europa kati ya Atletico na Marseille mnamo Mei 16 ilionyesha ukosefu wa heshima

Mnamo mwezi Januari, Barcelona ilikana madai kwamba ilikuwa imekubaliana na Griezmann ambaye anahudmia kandarasi yake hadi 2022 msimu huu .