Usajili

CHELSEA KURUDI KWA BEKI WA NAPOLI, TOURE HATAKI KUONDOKA ENGLAND

MATAJIRI wa Jiji la London Chelsea, wanawaza kurudi tena kuwania saini ya mlinzi wa kati wa SSC Napoli na timu ya taifa ya Senegal Kalidou Koulibaly anayekadiriwa kuwa na thamani ya €60m.

Chelsea wanamsaka nyota huyo kwa msimu wa pili sasa baada ya kutoswa katika dirisha la kiangazi lililopita na kwa sasa wamezidi kuvutiwa na shughuli anayoifanya ndani ya Serie A.

Kwa upande mwingine nyota mkongwe wa Manchester City na Cote de Voire, Yaya Toure, amesema kuwa hata akiachwa na kikosi hicho kama inavyoripotiwa, basi hataondoka katika Ligi ya nchi hiyo na badala yake atatafuta timu inayoshiriki ligi hiyo hiyo kwa msimu ujao.

Siku mbili zilizopota, kocha mkuu wa Man City Pep Guardiola, alitoa msimamo wake na kusema kuwa mkongwe huyo hataongezewa mkataba na atalazimika kuondoka mwishoni mwa msimu huu.