Usajili

NYOTA MAJIMAJI AWATIKISA BOCCO,OKWI

MSHAMBULIAJI Wa Majimaji FC, ya Songea, Marcel Boniventure 'Kaheza', amewabwaga Emmanuel Okwi pamoja na John Bocco, katika kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa mwezi April kunako Ligi kuu Tanzania Bara (VPL).

Kaheza ameshinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake kupata pointi saba katika michezo minne ndani ya mwezi huo, huku akifunga mabao saba ikiwemo mabao matatu 'Hat-trick', katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting mwishoni mwa Juma lililopita.

Mshambuliaji huyo anayekuja kwa kasi katika vita ya upachikaji mabao VPL, amewapita mastaa kadhaa wa klabu kubwa hapa nchini kwa sasa na kuwa nyuma ya Emmanuel Okwi mwenye mabao 19 na John Bocco aliyezama kambani mara 14, huku yeye akiwa na mabao 13 kibindoni.

Aidha taarifa za chini chini zinaeleza kuwa viongozi wa Simba wapo katika harakati za kuhakikisha wanapata saini ya staa huyo kwa ajili ya msimu ujao.