Usajili

EDINSON CAVANI ANAINGIA, ALVARO MORATA ANATOKA CHELSEA

Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata anaweza kuruhusiwa kwenda Juventus kisha klabu yake ikamsajili staa mwingine kutoka Ufaransa.

Imefahamika kuwa wababe hao wa Serie A wanamtaka Morata, 25, kwa mkopo kisha kuwe na kipengele cha kumsajili kwa pauni 43m baada ya kuonekana kutofurahia maisha ya England.

Hivyo, Chelsea yenyewe imeanza mchakato wa kumuwania Edinson Cavani wa Paris Saint-Germain ili kuziba pengo hilo.