Usajili

KOCHA MANCINI MBIONI KUSAINI MKATABA WA KUINOA ITALIA

TAARIFA ni kuwa Roberto Mancini amekubali ofa ya miaka miwili kusaini mkataba wa kuinoa Italia baada ya Carlo Ancelotti kuipotezea hiyo ofa.

Imeelezwa kuwa Mancini, 53, ambaye ni kocha wa zamani wa Manchester City anaweza kuanza kazi yake kuelekea mechi dhidi ya Saudi Arabia mnamo Mei 28 lakini atatangazwa kuchukua nafasi hiyo Mei 20.

Ancelotti hakuitaka ofa hiyo kwa kuwa nia yake ni kurejea ngazi ya klabu.