Usajili

VIGOGO WAMUWANIA BELLINI, ZIMO MAN UNITED, CHELSEA AU BARCELONA

Beki wa kulia wa Arsenal, Hector Bellerin, ameingia katika rads za timu tatu kwaajili ya usajilk majira ya kiangazi.

Muhispania huyo anawindwa na Klabu za Manchester United, Chelsea na walezi wake wa utotoni FC Barcelona ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakimuwinda.

Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa SPORT, umearifu kuwa mchezaji huyo anatarajia kuonfoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu na huenda akatua katika klabu moja wapo kati ya hizo huku FC Barcelona wakipewa nafasi kubwa kuweza kumrejesha kijana huyp nyumbani.