Usajili

KIUNGO CHELSEA AHITAJIKA WEST HAM

KLABU ya soka ya Westham United, yenye makazi yake London Uingereza, wanaangalia uwezekano wa kupata huduma ya kiungo wa Chelsea Danny Drinkwater.

Kwa mujibu wa Daily Telegraph, inarilotiwa kuwa wagonga nyundo hao wa London, wapo tayari kutoa kitita cha Pauni Milioni 30 (£30m), ili kupata huduma ya kiungo huyo wa kiingereza.

 

 Drinkwater alisajiliwa na Chelsea akitokea Leicester City, katika usajili wa dirisha dogo mwezi Januari mwaka huu.