Usajili

CANNAVARO KAULIZWA KUHUSU LWANDAMINA KUIKIMBIA YANGA, AMEJIBU HIVI...

Gumzo ndani ya Yanga ni kuhusu kuondoka kwa Kocha George Lwandamina ambaye imeelezwa kuwa ametua ndani ya Klabu ya Zesco United.

Kocha huyo ametua kikosini hapo ikiwa ni timu yake ya zamani kutokana na kile kinachoelezwa baadhi ya mambo kutokwenda sawa.

Alipoulizwa juu ya suala hilo, nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ameeleza kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo na wahusika ni uongozi wa timu.

Cannavaro alisema suala la kocha kuondoka ni ngumu yeye kulielezea zaidi viongozi wa klabu ndiyo wanauwezo wa kulisemea.

 “Masuala ya kocha kuondoka katika timu mimi ni nahodha lakini sipaswi kuzungumzia hilo wanaotakiwa kuzungumzia na viongozi wajuu ndiyo wanaolifahamu jambo hilo,” alisema Cannavaro.