Usajili

MABADILIKO AZAM FC, MZUNGU HATARINI KUSEPESHWA, BABU HAB VAN PLUIJM MGUU SAWA

Kutokana na mwenendo wa timu ya Azam FC kuendelea kutokuwa mzuri huku ikiachwa mbali katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, kuna mabadiliko yananukia ndani ya timu hiyo.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba ambaye ni raia wa Romania anaweza hasiongezwe mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo huku Kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm akitajwa kuchukua mikoba yake.

Inaelezwa kuwa Pluijm tayari amefikia makubaliano na uongozi wa Azam FC na wakati wowote anaweza kusaini mkataba kabla ya kutambulishwa.

Azam FC imedhamiria kuachana na Cioaba baada ya timu kushindwa kutwaa taji lolote Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo sasa.

Ikiwa dili litakamilika, basi Azam FC itakuwa timu ya tatu kwa Hans van der Pluijm kufundisha Tanzania baada ya Yanga na Singida United. 

Cioaba alijiunga na Azam FC, Januari mwaka jana akichukua nafasi ya Zeben Hernandez Rodriguez wa Hiapania, ameshinda taji moja moja tu, Kombe la Mapinduzi, Januari mwaka huu.