Usajili

BREAKING NEWS: KOCHA LWANDAMINA ‘ASEPA’ YANGA, AFUATA AJIRA MPYA

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina ameondoka nchini Tanzania na kuelekea kwao, Zambia.

Licha ya kuwa bado haijawekwa wazi sababu za safari hiyo lakini tetesi zinadai kuwa amekwenda kuzungumza na Klabu ya Zesco United ya kwao kuna uwezekano akatambulishwa rasmi kuwa kocha wa timu hiyo Alhamisi ya wiki hii.

Hakuna kiongozi wa Yanga aliyepatikana kuthibitisha juu ya suala hilo lakini kocha huyo hakutokea katika mazoezi ya asubuhi ya leo na wala hakutoa taarifa zozote kwa uongozi.

Ikiwa itakuwa ni kweli taarifa hizo, itakuwa pigo kwa Yanga kwa kuwa tayari imeshaonyesha mwelkeo wa kufuzu Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuifunga Wolaita Ditcha ya Ethiopia.

Lwandamina alijiunga na Yanga Novemba mwaka 2016 akichukua nafasi ya Hans van der Pluijm wa Uholanzi.