Usajili

MATAJIRI WA UFARANSA, PARIS SAINT GERMAIN WAMKOMALIA MOHAMED SALAH

Matajiri wa Ufaransa, Paris Saint Germain (PSG) wameongeza kasi ya kumuwania kumsajili kinara wa mabao wa Liverpool, Mohamed Salah katika usajili wa majira ya kiangazi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri, amekuwa kwenye kiwango  bora msimu huu akiwa amefunga mabao 29.

Salah mwenye miaka 25 alijiunga na Liverpool kutoka AS Roma ya Italia katika usajili wa majira ya kiangazi msimu uliopita.

Amefunga jumla ya mabao 38 katika michuano yote, akitoa pasi za mwisho mara 13 katika mashindano tofauti msimu huu.

PSG inasaka mfungaji hodari wa mabao kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji nguli Zlatan Ibrahimovic anayecheza Los Angeles Galaxy ya Marekani.