Usajili

YANGA: TUPO KAMILI, NJOONI UWANJANI LEO TUWAMALIZE STAND UNITED

Yanga wanatarajiwa kushuka uwanjani leo Jumatatu katika kipute cha Ligi Kuu ya Vodacom kukipiga dhidi ya Stand United.

Beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amesema kwamba ni muhimu mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani, kwani hiyo itawapa hamasa wapigane na kushinda leo.

Upande wa kipa chipukizi Kabwili yeye amesema kwamba mashabiki wa Yanga hawapaswi kujiweka nyuma, wanatakiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti wachezaji wao na akasema wao watapigana washinde mchezo wa leo. 

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi amesema kwamba ushindi leo ni muhimu na zaidi malengo yao ni ubingwa wa Ligi Kuu, hivyo amewaomba wapenzi wa Yanga wajitokeze uwanjani kwa wingi leo.

Yanga wanawakaribisha Stand United jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wakihitaji ushindi ili kurudi nafasi ya pili, kufuatia Azam FC kushinda 2-1 dhidi ya Mbao FC jana. 

Ushindi wa jana unaifanya Azam FC ifikishe pointi pointi 44, sasa ikiizidi Yanga pointi moja huku ikizidiwa pointi mbili na Simba iliyo kileleni kwa pointi 46, ingawa yenyewe imecheza mechi mbili zaidi.