Usajili

MBARAKA YUSUPH AWEKWA PEMBENI KWA MUDA AZAM FC

Baada ya kuumia katika mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC uliofanyika Alhamisi iliyopita, Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa amezungumzia afya ya mshambuliaji wa Azam FC, Mbaraka Yusuph.

Straika huyo aliumia wakati timu hiyo ikiichapa Mwadui bao 1-0 katika Ligi Kuu ya Vodacom, ambapo daktari huyo bingwa wa tiba za michezo amesema walimpumzisha kwa muda mchezaji huyo kabla ya kumuangalia hali yake baadaye.

“Mbaraka Yusuph alipata matatizo ya kugongwa katika msuli wa paja na ni maumivu na tumeendelea kumuangalia na kumpumzisha lakini Jumamosi (jana) tutajaribisha tena kumuangalia yupo katika hatua gani ya maumivu na kuanza mazoezi mepesi mepesi,” alisema.

Yusuph alishindwa kuendelea na mchezo huo dakika ya 24 tu baada ya majeraha hayo na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji Shaaban Idd.