Usajili

 JEMBE ULAYA ACHAMBUA KIPIGO CHA YANGA 

Bakari Malima maarufu kwa jina la Jembe Ulaya ameuzungumzia mchezo wa jana ambapo Yanga ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Township ya Botswana.

Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa ambapo timu hizo zitarudiana wiki moja na nusu ijayo.

Aliuchambua mchezo huo, Malima ambaye ni beki wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, alisema tatizo lililopo Yanga ni sehemu ya kiungo.

Amesema Yanga inatakiwa ifanye kazi ya ziada kurekebisha kasoro iliyojitokeza katika mchezo huo wa kwanza na kuamini kuwa wanaweza kufanya vizuri katika mchezo wa marudio kama watayafanyia kazi makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza.

Katika kipute hicho cha jana, bao la Yanga lilifungwa na Obrey Chirwa.