Usajili

MAN CITY YAMPONZA RIYAD MAHREZ, HALIPWI MSHAHARA KLABUNI KWAKE

Mshambuliaji wa Leicester City, Riyad Mahrez ameonywa kuwa hatalipwa mshahara wake wa pauni 100,000 kwa wiki ikiwa ataendelea na mgomo wake.

Mchezaji huyo amekuwa katika mgogoro na klabu yake tangu dili la kwenda Manchester City lilipokwama siku ya mwisho ya usajili mwezi uliopita.

Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England (PFA) kupitia kwa kiongozi wake, Gordon Taylor kinataka kuingilia suala hilo huku kikimuonyesha Mahrez kuwa atapoteza haki ya malipo yake ya mshahara ikiwa mgogoro huo utaendelea.