Usajili

KISA SANCHEZ, SASA DE GEA NAYE ANATAKA MSHAHARA MNONO MAN UNITED

 Mshambuliaji wa Manchester United, Alexis Sanchez ndiye mchezaji anayelipwa ghali kwenye Ligi Kuu ya England akiwa anachukua kitita cha pauni 500,000 kwa wiki.

Sasa baada ya dili hilo kuwa linafanya kazi, kipa wa Manchester United, David de Gea, naye yupo tayari kusaini mkataba mpya na timu hiyo ambao utamfanya awe analipwa kitita cha pauni 375,000 kwa wiki.

Mchezaji huyo anatarajiwa kuomba mkataba huo ambao utamfanya awe kipa anayelipwa ghali kwenye Ligi Kuu England.

Kipa huyo raia wa Hispania amekuwa akiwindwa mara kwa mara na Real Madrid na Manchester wanafahamu kuwa kama hawatampa mkataba huo basi anaweza kuondoka kwenye timu hiyo.

De Gea analipwa mshahara wa pauni 210,000 kwa wiki.