Usajili

COUTINHO AANZA KUTUPIA BARCELONA, ASISTI YA SUAREZ YAWEKA REKODI

Timu ya Barcelona imefanikiwa kufanya kweli na kufuzu kucheza fainali ya Kombe la Mfalme baada ya kuifunga Valencia mabao 2-0, jana usiku.

Kutokana na ushindi huo sasa Barcelona imefuzu kwa jumla ya mabao 3-0 kwa kuwa katika mchezo wa kwanza walipata ushindi wa bao 1-0.

Kiungo mshambuliaji mpya kikosini hapo, Philippe Coutinho alifunga bao lake la kwanza tangu atue Hispania hivi karibuni na kuwa msaada mkubwa kaytika timu hiyo kufuzu fainali ambapo sasa watakipiga dhidi ya Sevilla.

Mfungaji wa bao la pili katika mchezo huo alikuwa ni Ivan Rakitic aliyemalizia pasi nzuri ya Luis Suarez.

Rekodi ya kipekee ambayo iliwekwa katika mchezo huo ni kuwa Suarez ndiye ambaye alimpa pasi ya asisti Coutinho kufunga bao lake la kwanza wakiwa Liverpool mwaka 2013 walipicheza dhidi ya Swansea, pia safari hii Suarez pia ametoa asisti kwa Mbrazili huyo kufunga bao lake la kwanza akiwa Barcelona.