Usajili

MKONGWE PATRICE EVRA AFURAHIA MAISHA WEST HAM UNITED

Timu ya West Ham United inayonolewa na Kocha David Moyes imemsajili beki wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra.

Evra mwenye umri wa miaka 36, amejiunga na West Ham ikiwa ni siku chache baada ya kufukuzwa Marseille ya kwao Ufaransa baada ya kumvamia shabiki.

Beki huyo wa kushoto aliyewahi kung’ara na timu ya taifa ya Ufaransa pia, amekabidhiwa jezi namba 27 ambayo ilikuwa inavaliwa na Mfaransa mwenzake, Dimirti Payet.

Inakumbukwa Evra alitengeneza jina kubwa akiwa Monaco na Man United, tangu atimuliwe Ufaransa amekuwa akionekana katika mitandao ya kijamii akifanya mazoezi.

Mara baada ya kutua kikosini hapo, Evra ambaye ameshaanza mazoezi kikosini hapo ametumia ukurasa wake wa Instagrama kuelezea kufurahishwa kwake na kitendo cha West Ham kumsajili.