Usajili

ANTONIO CONTE NI MBISHI, ASEMA HANA HOFU YA KUFUKUZWA CHELSEA

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesema hana hofu yoyote juu ya kibarua chake licha ya timu yake kufungwa mabao 4-1 na Watfard, jana.

Kocha huyo yupo hatariuni ikiwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abromovich atachukua maamuzi juu yake kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.

Lakini Conte yeye amesema suala la kazi anawaachia mabosi wake kwani yeye binafsi amekuwa akijitoa kwa 120% kwa ajili ya timu hiyo na kinachotokea uwanjani ndio kama hivyo kinavyoonekana.

Conte amesema kuhusu kibarua chake yeye anaona yuko poa tu na Chelsea lakini kama wenyewe Chelsea wataona kwamba hafai kuendelea kukaa klabuni hapo baasi ataondoka tu lakini hana wasiwasi.

Antonio Conte amesisitiza kwamba yeye hakoseshwi usingizi na tetesi za kufukuzwa kazi na amesema yeye anaona anafanya vizuri kwa ajili ya Chelsea ila kama wataona vinginevyo baasi watafanya lililo sahihi.

Mara ya mwisho kwa Chelsea kukubali kipigo mfululizo cha mabao 3+ katika EPL ilikuwa mwaka 1995 walipopigwa na United 1-4, kisha wakapigwa na Blackburn 0-3, kwa hiyo jana inakuwa mara ya kwanza kufanywa hivyo tangu 1995.