Usajili

GOLDEN STATE YACHAPWA NA CLIPPERS, KELVIN DURANT AKIWEKA REKODI 

Mabingwa watetezi wa ligi ya kikapu nchini Marekani (NBA), Golden State Warriors, alfajiri ya leo walipoteza mchezo wao wa ligi hiyo dhidi ya Los Angeles Clippers baada ya kufungwa kwa vikapu 125-126 dhidi ya Clippers ikiwa ni mchezo wao wa tisa kupoteza katika msimu huu.

Katika mchezo huo uliochezwa katika Dimba la Staples Center katika ndani ya Los Angeles, Golden State iliwakosa nyota wake wawili Steph Curry ambaye ni majeruhi pamoja na Klay Thompson ambaye kwa mujibu wa mwalimu wa timu hiyo, Steve Kerry, alikuwa nje kutokana na kupumzishwa sababu amecheza michezo mingi.

Upande wa Clippers wao wamemkosa nyota wao, Andy Griffing ambaye alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Lakers pamoja na Garrinali.

Katika mchezo huo imeshuhudiwa mchezaji wa Clippers, Louw Williams akifunga jumla ya vikapu 50 ambapo vikapu 30 amefunga katika robo ya tatu ya mchezo huo ikiwa ni rekodi ya peke yake kufunga vikapu vingi katika robo ya tatu akitokea benchi na kuiwezesha timu yake kushinda katika mchezo huo.

Wakati huohuo, nyota wa Golden State, Kelvin Durant ameendelea kuwa msaada mkubwa katika timu hiyo baada ya kufunga jumla ya vikapu 40, mirejesho 4 na pasi 4, licha ya timu yake kupoteza mchezo huo na kufanikiwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo katika ligi hiyo kufikisha jumla ya vikapu 20,000 japo LeBron James wa Cleveland Cavaliers alikuwa akiishikilia rekodi hiyo na kuingia katika orodha ya wachezaji 40 waliofikisha jumla vikapu 20,000 katika historia ya ligi hiyo NBA.

Katika matokeo mengine Oklahoma City Thunder imepoteza mchezo wake wa pili mfululizo baada ya alfajiri ya leo kufungwa na Timberwolves kwa jumla ya vikapu 88-104 huku nyota wa timu hiyo [Mr triple Double), Russel Westbrook akifunga vikapu 38 mirejeo 10 na pasi 5 licha ya timu yake kupoteza

Orlando Magic wamepoteza mchezo wao dhidi ya Milwaukee Bucks baada ya kufungwa jumla ya vikapu 103-110.

New Orlens Pelican wao wakachapwa na Memphis Grizzlies kwa jumla ya vikapu 102-105, Portland Trail Blazers wakapoteza mchezo wao nyumbani dhidi ya wabishi wa Magharibi Houston Rocket kwa jumla ya vikapu112-121 huku Chicago Bulls wakiweza kuwafunga Newyork Knicks kwa vikapu 122-119, Dentroit Piston wao wakawalaza mabishoo wa Brooklyn Nets kwa vikapu 114-80.

Uttah Jazz wamewachapa Washington Wizards kwa vikapu 107 dhidi ya 104, Miami Heat wakawafunga Indiana Pacers vikapu 114 kwa 1o6, Dallas Mavericks wakawachapa Charlotte Hornets 115 kwa 111 na mchezo wa mwisho Atlanta Hawks wamewafunga Denver Nuggets vikapu 110 kwa 97.