Usajili

HANS POPPE AWAJIA JUU MKUDE, KICHUYA

 Sekeseke la wachezaji mastaa wa Simba, Jonas Mkude na Shiza Kichuya kupanda jukwaani kukaa mara baada ya kutolewa uwanjani wakati timu hiyo ilipokuwa ikicheza dhidi ya URA, kumemubuak kigogo wa Simba.

Mwenyekiti  wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba,  Zacharia Hans Poppe ameamua kufunguka juu ya kilichotokea kwa wachezaji hao na kuweka wazi kuwa ni wazi kuna tatizo la nidhamu kikosini hapo.

Mkude na Kichuya walitolewa uwanjani na Kocha Masoud Djuma wakati wa mchezi wa Kombe la Mapinduzi walipocheza dhidi ya URA, Jumatatu ya wiki hii, mchezo ambao ulimalizika kwa Simba kupoteza kwa bao 1-0.

Akifafanua juu ya tukio hilo, Hans Poppe alisema hajajua tatizo hasa ni lipi lakini kama kuna sintofahamu zinatokea mpaka mchezaji anatoka anakwenda kwa watazamaji badala ya kwenda kwenye benchi basi kuna tatizo la kinidhamu.

Hans Poppe amesema inapotokea mchezaji anafanyiwa mabadiliko halafu asirudi kwenye benchi badala yake akaenda kwa watazamaji ni ishara ya mgomo, inaonyesha kama hakuridhika na maamuzi ya mwalimu, ni kitu ambacho kitashughulikiwa kujua tatizo ni nini kwa sababu si kitu cha kawaida.