Usajili

HII NDIYO HABARI MPYA YA SHOMARI KAPOMBE NDANI YA SIMBA

Baada ya kuwa nje kwa miezi kadhaa sasa, Shomari Kapombe ambaye ni beki wa Simba tayari ameanza

mazoezi mdogo mdogo katika mchakato wa kurejea kikosini hapo.

Akiwa nje ya uwanja kuna wakati Kapombe alirushiana maneno na mmoja wa vigogo wa klabu yake aliyedai kuwa mchezaji huyo kama anaona hawezi kucheza ni bora aondoke kuliko kuendelea kulipwa fedha huku akiwa nje ya uwanja muda mwingi.

Kocha wa Simba, Masoud Djuma amesema hatamtumia mchezaji huyo hadi atakapokuwa fiti.

Kapombe alianza mazoezi siku chache zilizopita wakati ambapo timu yake ikiwa bado ipo Visiwani Zanzibar inaposhiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Shuti Kali ambayo imewekas kambi Zanzibar kwa ajili ya michuano hiyo imezungumza na Kocha Djuma ambaye amesisitiza kuwa Kapombe anaendelea na mazoezi binafsi ya fitinesi kwa ajili ya kurejesha pumzi na stamina kabla ya kuanza kumtumia.

Djuma alisema beki huyo yupo kwenye mipango ijayo ya mashindano watakayoshiriki kwani ni lazima afanye programu hiyo ya mazoezi ili aendane na kasi ya wachezaji wenzake.