Usajili

MSUVA ATAJA KITAKACHOMUONDOA MOROCCO ANAKOCHEZA SOKA LA KULIPWA

Mtanzania Simon Msuva  ambaye anamilikiwa na timu ya Diffaa Al Jadida ya Morocco amefunguka kuwa kitu pekee ambacho kitamwezesha yeye kuondoka nchini humo na kwenda

levo za juu kucheza soka ni juhuzi zake kuendelea kuwa za kiwango cha juu.

Staa huyo ambaye amefunga mabao matano kwenye Ligi Kuu ya Morocco kati ya mechi 14 alizocheza yupo nchini Tanzani ambapo amekuja kwa ajili ya mapumziko.

Amesema kuwa, moja ya mikakati yake ni kuona anafanikiwa kuvuka mipaka zaidi ya kucheza nje ya Afrika, hivyo anatumia  kipindi hiki kuhakikisha anafanikiwa kuonyesha juhudi ili kufikia malengo.

Amesisitiza kuwa anaamini atatimiza malengo kwa kuwavuta mawakala kutokana na uwezo anataounyesha, anafurahia mazingira kwa kuwa anapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wenzake.