Usajili

TIMU 5 ZENYE UKUTA MGUMU ZAIDI KWENYE LIGI KUU YA VODACOM

Wakati Ligi Kuu ya Vodacom ikiwa imesimama kwa muda kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi, tujikumbushe timu ambazo zimefungwa mabao machache katika ligi hiyo.

Hadi sasa timu zote zimeshacheza michezo 12 katika msimu huu wa 2017/18:

AZAM FC: Ndiyo timu yenye safu kali ya ulinzi kwenye Ligi Kuu kwanii katika mechi 12 wameruhusu magoli matatu tu hadi sasa

SIMBA: Wameruhusu nyavu zao kuguswa mara 6 tu katika mechi 12 hadi sasa

SINGIDA UNITED: Ni moja ya timu yenye safu bora ya ulinzi kwenye Ligi, wamefungwa magoli 6 pekee katika mechi 12

MTIBWA SUGAR: Wameruhusu goli 6 tu katika michezo 12 ya Ligi Kuu ni Azam pekee aliyefungwa magoli machache kuliko Mtibwa

YANGA: Wameruhusu nyavu zao kuguswa mara sita katika mechi 12 za Ligi Kuu